Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Kawaida · Kidato cha Tatu

Kiswahili

Mikabala ya uainishaji ngeli za nomino

takriban dakika 5 kusoma

Mada za sehemu hiiNgeli Za NominoMada 2
  1. Fasili ya ngeli
  2. Mikabala ya uainishaji ngeli za nomino

MSINGI WA KUTUMIA VIAMBISHI VYA UPATANISHO WA KISARUFI

  1. Upatanisho wa kisarufi ni utaratibu wa kupatanisha viambishi vya maneno ili kuleta mshikamano wa maneno katika tungo.
  2. Upatanisho wa kisarufi katika Kiswahili hujitokeza zaidi kati ya nomino au kiwakilishi na kivumishi na kati ya nomino au kiwakilishi na kitenzi.
  3. Mtazamo huu wa uanishaji ngeli ambao umefuatwa na Nkwera (1978), Taasisi ya Elimu (1988), na Kapinga Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili wa kisarufi kati ya nomino na viambishi awali.
  4. Vilivyo katika vitenzi yaani vipatanishi kwa mujibu wa mtazamo huu, ngeli za majina ya Kiswahili ni 9 kama ifuatavyo.
NAMBAVIAMBISHIAWALI VIPATANISHIMFANO
i.YU – A – WAYU – A – (Umoja) WA – (wingi)1. Mtu anakuja 2. Watu wanakuja
ii.U – IU – (Umoja) I – (Wingi)1. Mti umeanguka – miti imeanguka 2. Mto umefurika – mito imefurika 3. Mguu unauma – miguu inauma
iii.LI – YALI – (Umoja) YA – (Wingi)1. Jicho linaauma – macho yanauma 2. Panga linakata – mapanga yanakata
iv.KI – VIKI – (umoja) VI – (Wingi)1. Kisu kinakata – visu vinakata 2. Chakula kimechacha – vyakula vimechacha
v.I – ZII – (Umoja) ZI – (Wingi)1. Kalamu imekatika - kalamu zimekatika 2. Nyumba imeanguka - nyumba zimeanguka
vi.U – ZIU – (Umoja) ZI – (Wingi)1. Ufa unazibwa – nyufa zinazibwa 2. Ukuta umejengwa – kuta zimejengwa
vii.U – YAU- (Umoja) YA – (Wingi)Ugonjwa umeenea – magonjwayameenea
viii.KUKU – (Umoja)1. Kuimba kunafaa 2. Kucheza kunachosha
ix.PA – MU – KUPA – MU – KU –1. Mahali pale panafaa 2. Mahali mule mnafaa 3. Mahali kule kunafaa

MSINGI WA KUTUMIA KIAMBISHI CHA NOMINO NA KIAMBISHI CHA UPATANISHO WA KISARUFI

  1. Utaratibu huu wa uanishaji wa ngeli unaozingatia viambishi vyote viwili yaani viambishi vya nomino na viambishi vya upatanishi wa kisarufi kutokana na tatizo/ matatizo yaliyojitokeza katika mtazamo wa kutumia kiambishi cha kisarufi peke yake bila kuhusisha nomino zake za awali.
  2. Mfano wa utaratibu huu wa uainishaji ngeli za Kiswahili sanifu ni;
NAMBAVIAMBISHIJINA LA NGELIMFANO
1.MU – AMuuguzi anasoma
2.WA – WAWatu wanalima
3.M – UMti umeanguka
4.MI – IMiti imeanguka
5.JI/Q – LIJiwe limeondolewa (Q) Panga limenolewa
6.MA – YAMajani yamefagiwa Mawe yameanguka
7.KI – KIKiti kimevunjika
8.VI – VIViti vimevunjika
9.N/Q – N/QNyumba zinapendeza (Q) mboga zinapikwa
10.N/Q – ZINyumba zinapendeza (Q) mboga zinapikwa
11.(L) U - (L)UUbao umeanguka
12.M – ZIMbao zimeanguka
13.KA – KAKavulana kamekuja
14.U – UUgonjwa umeingia
15.KU – KUKuimba kumeendelea
16.MA – MAMahali mnapotoa
17.MA – KUMahali kunakofaa

KASORO/ UDHAIFU/ MATATIZO/ YANAYOJITOKEZA KATIKA UANISHAJI WA NGELI

  1. Wanamapokeo au wataalamu walioainisha ngeli katika misingi ya kuangalia umoja na wingi tatizo lao kuu ni kwamba wamechanganya majina ya viumbe hai na visivyo hai katika ngeli zao. Mfano katika ngeli ya KI – VI, hapa wamechanganya na kuingiza majina ya vitu vilivyo hai na visivyo na uhai. Mfano; kipepeo, kipofu, kiziwi, kilema. Hii ni kutokana na dhana yao na kuanisha ngeli katika jozi ya umoja na wingi na kuangalia viambishi awali katika nomino.
  2. Kuna majina mengine hayana ngeli zake. Tukitazama hasa katika uanishaji wa 1 na 2, mfano majina ya vimiminika kama vile maji, maziwa, mafuta n.k. Japokuwa wameweza kulitatua hili kwa kuweka maneno/ majina haya katika ngeli ya Ji/Q – Ma; katika sehemu ya vitu visivyohesabika na visivyokuwa na wingi
  3. Kuna baadhi ya ngeli huwa zinawakilishwa vilevile. Mfano ngeli ya 9 na 10, vyote vinawakilishwa na kiambishi N ambacho katika mazingira ya kawaida hujulikana kama (ny-) pia ngeli ya 11 na 14 zinawakilishwa na kiambishi U- na ngeli za 15 na 17 zote zinawakilishwa na kiambishi Ku-
  4. Kuna baadhi ya majina hayakubali kuwekwa katika makundi ya umoja na wingi. Mfano; sisimizi, nyama, maiti, ndizi, ndama, panzi, simba n.k.
  5. Kwa kigezo cha upatanishi wa kisarufi, muainisho huu unaongelea ngeli za nomino lakini hazigusii nomino zenyewe moja kwa moja bali unatumia tu upatanishi wake wa kisarufi
  6. Pia kwa upande mmoja ngeli zinahesabiwa katika jozi za umoja na wingi, lakini kwa upande mwingine zimehesabiwa katika ngeli moja moja Mfano; katika ngeli ya 2, 6 na 7 (katika umoja) zote zimewakilishwa na kiambishi Zi- ni wazi kwamba hili ni tatizo
  7. Ngeli ya kwanza imepewa viambishi viwili vya YU – na A – , lakini ukweli ni kwamba matumizi ya kiambishi cha YU – ni ya kilahaja zaidi kuliko ya Kiswahili sanifu. Si jambo la kawaida kukuta wasemaji wa Kiswahili sanifu wakisema kitu kama, "mwalimu yu afundisha. Mtoto yu aja, mzee yu azeeka" n.k kwa misingi hiyo basi tunasema kiambishi hiki kisitumike. Hata hivyo pengine ni muhimu kusema katika Kiswahili sanifu matumizi haya ya Yu – hujitokeza katika vivumishi vya maneno yupi, huyu n.k
  8. Ukweli ni kwamba ngeli za 16, 17 na 18 ni ngeli za mahali kwa hivyo kiambishi halali katika ngeli zote hizi 3 ni Mu – na wala si Pa – Mu – ku – kama ilivyoelezwa kimapokeo.Tunasema ni Ma – kwa sababu ukiyachunguza maneno mahala, pahali, utaona kwamba katika mifano iliyotolewa katika uanishaji yote yanahusu mahali

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza