Mada za sehemu hiiMaendeleo Ya KiswahiliMada 2
- Asili ya Kiswahili
- Kukua na kueneo
Kukua na kueneo kwa Kiswahili nchini Tanzania
Hali ya awali ya Kiswahili
- Kiswahili kilikuwepo kabla ya wageni kufika.
- Kilitumika kama lugha ya mawasiliano na biashara miongoni mwa wenyeji wa Pwani ya Afrika Mashariki.
Mtazamo wa Wageni kuhusu Kiswahili
- Wageni walipofika, hawakuona sababu ya kutumia lugha nyingine kwani Kiswahili tayari kilikuwa kinaeleweka.
- Kiswahili kilitumika kwa urahisi katika shughuli za kibiashara, kijamii, na kiutawala.
Wageni waliofika Pwani ya Afrika Mashariki
- Waarabu
- Wareno
- Wajerumani
- Waingereza
Mchango wa Wageni kwa Kiswahili
- Wengine walikiendeleza Kiswahili, kwa kukitumia katika utawala, elimu, na biashara.
- Wengine walikidumaza Kiswahili, kwa kuingiza lugha zao au kukipunguza hadhi yake.
Kukua na kueneo kwa Kiswahili enzi za Waarabu
Kuenea kwa lugha ni kuongozeka kwa watumiaji. Wageni wa kwanza kuja pwani ya Afrika mashariki ni Waarabu na kutokana na kuingiliana na wabantu katika nyanja mbalimbali Kiswahili kilichukuliana maneno na kuathiriana na lugha ya Kiarabu. Sababu zilizochangia kukua kwa Kiswahili enzi za Waarabu:
- Biashara: Waarabu walipowasili katika mwambao wa pwani ya Afrika mashariki walianza kufanya biashara na wabantu. Kutokana na maingiliano hayo Kiswahili kilianza kupanuka na kuongozeka misamiati kwa hiyo bila shaka Kiswahili kilikuwa kutokana na maingiliano hayo. Mfano wa msamiati uliochukuliwa kutoka kwa Waarabu ni kama vile jahazi, kodi, adesii n.k.
- Utawala: Waarabu pia walitumia Kiswahili katika shughuli mbalimbali za kiutawala. Waarabu walitawala Zanzibar, sehemu za pwani ya bara na Pemba. Kutokana na shughuli za kiutawala kuna maneno ya Kiarabu ambayo yameingia kwenye Kiswahili. Mfano: mwinyi, sultani, mtukufu, enzi n.k.
- Dini: Hali kadhalika walipowasili walianzisha dini yao ya Kiislamu kwenye upwa wa Afrika kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Waafrika walifundishwa kuandika na kusoma kwa hati za Kiarabu ili waweze kusoma na kuelewa Kurani. Hivyo wakajikuta wanaingiza baadhi ya maneno ya Kiarabu kwenye lugha ya Kiswahili. Baadhi ya maneno ni kama vile elimu, alasiri, alfajiri n.k.
- Ndoa: Wageni hawa pia walipofika pwani ya Afrika mashariki waliishi kwa miaka mingi na hivyo kuchangamana na wenyeji na baadae Waarabu wakaoa wanawake wa Kibantu na hata vizazi vyao vilipozaliwa. Walitumia lugha ya Kiswahili katika mawasiliano yao na pia hata utamaduni wao ulijiegemeza kwenye lugha ya Kiswahili. Hata jamii ya watu wa pwani waliwaita watoto wao Waswahili badala ya maneno kama vile chotara, kwahiyo kutokana na hivyo basi ndoa kati ya Waarabu na Wabantu ulichangia kwa kiasi kikubwa kukua na kuenea kwa Waswahili.
Kukua na kueneo kwa Kiswahili enzi za utawala wa Wajerumani nchini Tanzania
- Urefu wa utawala
- Wajerumani walitawala Tanganyika kwa takriban miaka 30.
- Hali ya Kiswahili walipofika
- Walikuta Kiswahili kimekua sana na kinatumika katika sehemu nyingi za Afrika Mashariki.
- Matumizi ya Kiswahili na Wajerumani
- Kiswahili kilitumika kama chombo cha mawasiliano rasmi katika shughuli za utawala.
- Lugha hiyo ilitumika katika elimu, hasa kwa kutoa mafunzo ya awali.
- Mahitaji ya lugha kwa ajira
- Mfanyakazi wa Kiafrika alilazimika kujua Kiswahili kwa kuandika na kuongea ili kupata ajira.
- Ripoti zote za utawala wa Wajerumani ziliandikwa kwa Kiswahili.
- Usambazaji wa wahitimu
- Wanafunzi waliohitimu walitumwa kufanya kazi sehemu mbalimbali nchini, jambo lililosaidia kusambaza Kiswahili zaidi.
- Maeneo ya kilimo na lugha ya kazi
- Mashamba ya Wajerumani yalikuwa na wafanyakazi kutoka makabila tofauti.
- Kiswahili kilitumika kama lugha ya mawasiliano kati yao.
- Hili lilipelekea uchangiaji wa msamiati kutoka lugha za makabila mbalimbali katika Kiswahili.
Mbinu zilizotumika kueneza Kiswahili nchini Tanzania wakati wa utawala wa Wajerumani
-
Mahakama Utawala wa Kijerumani ulitumia pia lugha ya Kiswahili katika shughuli zake kwa hivyo kazi zote ziliendeshwa kwa lugha ya Kiswahili na pia wafanyakazi na wazee mahakani walihoji na kutoa hukumu kwa watuhumiwa kwa kutumia lugha ya Kiswahili na hivyo kuchangia kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili.
-
Elimu Mashuleni pia Kiswahili kilitumika kama lugha ya kufundishia na Kijerumani kilifundishwa kama somo la kawaida tu katika shule za msingi. Wajerumani walijenga shule sehemu za Tabora, Ujiji, Kilimatinda, Mpwapwa, Kasangu mwaka 1905, Iringa, Mwanza, Bukoba, Kilosa, Tukuyu na Moshi. Pia vyuo vya kufundishia walimu vilianzishwa huko Tabora na Bukoba hivyo basi walimu na wanafunzi walijifunza na kukitumia Kiswahili katika shughuli zao za elimu na kusababisha kuenea na kukua kwa Kiswahili.
-
Utawala Wajerumani walipofika nchini walikuta lugha ya Kiswahili imekua na kuenea sana hivyo nao katika utawala na hivyo kuamua kujifunza Kiswahili kabla ya kuja nchini na pia hapa nchini Wajerumani walitoa mwongozo kwa viongozi wa nchini kwa kutumia lugha ya Kiswahili na hivyo viongozi wote wa Kiafrika mfano akida, jumbe n.k walitakiwa kujifunza lugha ya Kiswahili kwasababu walikuwa wanatumwa sehemu mbalimbali sio nchi walikozaliwa tu hivyo kuchangia kukua na kuenea kwa haraka.
-
Shughuli za kilimo (mashamba) Wajerumani pia walianzisha mashamba makubwa ya mazao ya biashara na kuwalazimisha watu wafanye kazi kwenye mashamba hayo mfano, mashamba ya katani Tanga, Kahama, Kilimanjaro kwahiyo kwenye mashamba hayo kulikuwa na idadi kubwa ya watu kutoka sehemu mbalimbali na lugha yao ilikuwa ni Kiswahili kwahiyo wale waliobahatika kurejea majumbani mwao walisaidia kukieneza Kiswahili kwasababu waliendelea kutumia lugha ya Kiswahili.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza