Mada za sehemu hiiKadi Za MwalikoMada 1
- Kadi za Mwaliko
Kadi za Mialiko
Kadi za mialiko ni karatasi gumu lenye taarifa fupi za kumwalika mtu kuhudhuria sherehe au kikao fulani.
Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Uandishi wa Kadi za Mialiko
- Jina la mwandishi na anwani yake
- Jina la mwandikiwa
- Lengo la mwalikaji kwa ufupi
- Tarehe ya mwaliko
- Mahali pa kukutana
- Wakati wa kukutana
- Jibu lipelekwe kwa nani
Aina za Kadi za Mialiko
1. Kadi za Mwaliko Usio Rasmi
Hizi ni kadi zinazohusu mialiko ya kindugu au marafiki. Kadi hizi hazitaji vyeo vya waalikwa, bali huanza na maneno kama vile Bwana, Bibi, Ndugu, n.k.
Mfano wa Kadi ya Mwaliko Usio Rasmi
MWALIKO WA KIKAO
Familia ya Bibi Mwanaheri Mchele wa Kinondoni B, Dar es Salaam, inayo furaha kukualika kwenye kikao cha Kitchen Party ya binti yao mpendwa Nyamchele, kitakachofanyika siku ya Jumamosi, tarehe 25/02/2021, saa 10:00 jioni, nyumbani kwake Kinondoni B.
Kufika kwako ndiyo mafanikio yetu!
Mawasiliano: 📞 Mwanaheri Kidawa: 0713 000000 📞 Husna Rajabu: 0714 000000
2. Kadi za Mwaliko Rasmi
Hizi ni kadi zinazohusu mialiko ya kiofisi, harusi, au sherehe mbalimbali za hadhi ya juu. Katika uandishi wake, majina huambatana na vyeo kama vile:
- Profesa
- Mchungaji
- Daktari
- Askofu
- Sheikh
- Mwalimu, n.k.
Mfano wa Kadi ya Mwaliko Rasmi
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM Fakulti ya Sayansi na Teknolojia
MWALIKO MAALUM
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinayo heshima kumwalika Profesa Juma Rajabu kuhudhuria kongamano la sayansi na maendeleo litakalofanyika tarehe 10 Mei 2025, kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Ukumbi wa Mikutano, Jengo la Sayansi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Tafadhali thibitisha uwepo wako kwa: 📩 Email: udsasayansi@udsm.ac.tz 📞 Simu: 0756 000000
Swali
Ni mambo gani muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa kadi ya mwaliko?
Ingia ili kuwasilisha jibu lako na lihesabiwe katika umahiri wako.
Ingia ili kufanya mazoeziMwalimu
Umekwama? Niulize chochote kuhusu mada hii.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu swali hili.
Ingia ili kuuliza