Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Kawaida · Kidato cha Kwanza

Kiswahili

Aina za kamusi

takriban dakika 3 kusoma

Mada za sehemu hiiAina Za ManenoMada 10

MATUMIZI YA KAMUSI

Kamusi ni kitabu cha maneno yaliyopangwa kwa utaratibu wa kialfabeti na kutolewa maana na maelezo mengine. Kitabu hiki huwa na idadi kubwa ya maneno kutoka katika lugha husika, na maneno hayo hutolewa maana na maelezo kwa lugha hiyohiyo au kwa lugha nyingine.

MUUNDO WA KAMUSI

Kamusi yoyote ile imegawanyika katika sehemu tatu nazo ni;

  1. Mwongozo wa msomaji (Utangulizi wa kamusi)
  2. Vifupisho na matumizi ya alama
  3. Kamusi yenyewe (orodha ya kamusi)

Mwongozo wa msomaji

Ni sehemu ambao unalenga kumuelezea mtumiaji wa kamusi ili aweze kutumia kamusi hiyo bila kupata usumbufu. Mwongozo wa msomaji huhusika na mambo yafuatayo;

  • Taarifa zilizoingizwa kam vile;
    • Vidalizo
    • Vibadala vya vidalizo
  • Kategoria ya maneno
    • Nomino
    • Vitenzi
    • Vielezi
    • Vivumishi
    • Umoja na wingi n.k
  • Maneno na utumizi wa maneno, mfano; Nomino (sarufi), Elementi (kemia)
  • Mifano ya matumizi
  • Lugha kienzo

Vifupisho na matumizi ya alama

Ni muhimu kwa mtumiaji wa kamusi kupata taarifa zinazohusu matumizi mbalimbali ya vifupisho, tarakimu, herufi na maana.

Mfano;

  • agh – aghalabu
  • ele – elekeza
  • fiz – fizikia
  • Kb – kibaharia
  • Kd – kidini
  • Kh – kihusishi
  • K.v – kamavile
  • Kv – kivumishi
  • Mt – methali
  • nh – nahau
  • n.k – Na kadhalika

Kamusi yenyewe

Hii ni sehemu ambayo inakuwa na orodha ya maneno mbalimbali yenye maana na ufafanuzi wa neno husika. Sehemu hii ndio kiini cha kamusi.

UFAFANUZI WA ISTILAHI MUHIMU KATIKA MADA HII YA UTUMIZI WA KAMUSI

Ni vema kufahamu istilahi kuu katika kujadili mada hii. Istilahi hizo ni hizi zifuatazo;

  1. Kidahizo
  2. Kitomeo
  3. Lugha kienzo

Kidahizo

Kidahizo ni neno lilioingizwa katika kamusi ili lipatiwe:

  • Maana
  • Ufafanuzi mwingine wa kisarufi (k.m. kimatamshi, kimuundo)
  • Ufafanuzi wa kimatumizi

Vidahizo huandikwa kwa kukolezwa wino ili kuonekana tofauti na maelezo yake.

Mfano wa Kidahizo

abee! au bee! – (kwa wanawake) ni neno la kuitika wanapoitwa.

Mpangilio wa Vidahizo

  1. Vidahizo huwa ni-pangwa kwa kufuata utaratibu wa kialfabeti.
  2. Tofauti za kimuundo baina ya aina moja ya neno na nyingine huchukuliwa kama msingi wa upangaji.
  3. Mpangilio huu hurahisisha kutafuta maana na matumizi ya neno katika kamusi.

Kitomeo

Kitomeo ni kidahizo pamoja na maelezo yake yote. Kitomeo kinaweza kuwa na maana, matumizi, na ufafanuzi wa kisarufi.

Mifano ya Kitomeo

  1. Maalimu – Mtu mwenye elimu kubwa ya dini ya Kiislamu.
  2. aathari – Masalio ya vitu na utamaduni wa watu fulani.
  3. abaa! – Neno la kumwita rafiki, mfano: Alaa! Aisee!
  4. abadani! – Neno linalosisitiza jambo kwa ufupi, ufasaha, utoshelevu, na uwazi.

Lugha kienzo

Lugha kienzo ni mtindo wa kutoa fasihi ya vidahizo kwa njia fupi na wazi. Hutumika katika kamusi kuwasilisha maelezo:

  • Kwa ufupi
  • Kwa ufasaha
  • Kwa utoshelevu
  • Kwa uwazi

Hutumika alama maalum ili kufupisha maelezo marefu au fasihi mbalimbali.

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza