Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Kawaida · Kidato cha Kwanza

Kiswahili

Aina za fasihi

takriban dakika 1 kusoma

Mada za sehemu hiiFasihi Kwa UjumlaMada 6

AINA ZA FASIHI

Kuna aina mbili (2) za fasihi

  1. Fasihi andishi
  2. Fasihi simulizi

i. FASIHI SIMULIZI

Ni fasihi ambayo hutumia masimulizi ya mdomo kufikisha ujumbe wake kwa jamii. Ni fasihi ambayo ni kongwe na ilianza tangu binadamu alipoanza kuishi duniani.

FASIHI SIMULIZI INA TANZU NNE NAZO NI

  1. Hadithi
  2. Semi
  3. Ushairi
  4. Maigizo

ii. FASIHI ANDISHI

Ni fasihi ambayo hutumia maandishi ili kufikisha ujumbe kwa jamii

Fasihi andishi ina tanzu nne

  1. Tamthilia
  2. Ushairi
  3. Ngonjera
  4. Riwaya

TOFAUTI KATI YA FASIHI SIMULIZI NA FASIHI ANDISHI

NAFASIHI SIMULIZIFASIHI ANDISHI
iHuwasilishwa na fanani kwa njia ya masimulizi au mdomoHuwasilishwa kwa maandishi kwa njia ya maandishi
iiHuifadhiwa kichwani na kusambazwa na mdomo au mazungumzoHuifadhiwa kwa maandishi na kusambazwa kwa maandishi
iiiHuruhusu mabadiliko ya papo kwa papoHairuhusu mabadiliko ya papohapo kazi ikishaandikwa haibadiliki hadi toleo jingine
ivIna tanzu nne kama vile Hadithi, Semi, Ushairi na MaigizoIna tanzu nne kama vile Tamthilia, Ushairi, Ngonjera na Riwaya
vHadhira yake ni watu wale katika jamii, watoto, wazee na wasomiHadhira yake ni watu wale wanaojua kusoma na kuandika
viIna umri mkubwaIna umri mdogo, imekuwepo baada ya ugunduzi wa maandishi
viiNi rahisi kusahau baadhi ya vipengeleSi rahisi kusahauliwa baadhi ya vipengele kwani imehifadhiwa kwa maandishi
viiiMuundo wake ni wa moja kwa mojaMara nyingi muundo wake ni wa mchangamano unaruhusu urejeshi
ixHuenda na wakati na mabadiliko ya matukio katika jamiiHaiendi na wakati kwa sababu ikishaandikwa haiwezi kubadilishwa

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza